Sunday, June 4, 2017

TABIA HUVUTA MAZINGIRA UYATAKAYO.

                             Tokeo la picha la HOW CHARACTER PULL YOU TO YOUR SUCESS QUOTES
Habari mpenzi mfuatiliaji wa makala hizi za APPLICATION ya LAZAROSAMWEL  namatumaini wiki hii  ni wiki ya matunda na wiki ya kukufanya kuwa mpya katika maisha yako.TWENDE PAMOJA kuanza hii wiki salama salmini.
 “Haujitengenezei mazingira ila unayachukua mazingira flani kutokana na tabia yako ulivyoijenga. Yani Tengeneza tabia na utachukua mazingira ambayo yanaendana na tabia yako uliyoitengeneza. Ukiwa mvivu utapokea mazingira na matokeo ya kivivu, ukiwa msengenyaji utayachukua mazingira sawa na ulivyo, kila kitu tayari kilishatengenezwa lakini sisi ni kuvichukua tuu kwa tabia zetu. Ni maamuzi yako na sio ya mtu mwingine kwamba unataka vipi? “-Lazaro Samwel  
Imam mmoja kwa jina la Hasan Ali Shah wa Nizari Ismailis  aliwahi kusema kwamba “Usimwambie Mungu wako changamoto zako kubwa kiasi gani,ziambie changamoto zako Mungu wako ni mkubwa kiasi gani”. Nami ningependa kukwambia kwamba changamoto ambazo huwa tunakutana nazo huwa tunazivisha sifa ambazo sio katika maisha yetu mpaka zinageuka kuwa matatizo na kila kukicha tunasahau uwepo wa Mungu mana hata tukiwa tunasali kitu ambacho kinatawala ni kuombea matatizo na sio kumwomba Mungu kutupa  nguvu ya kuweza kushinda changamoto ambazo tunakutana nazo. Sisi binadamu huwa na mtindo wa kumwachia Mungu kila kitu tena kwa kurelax na kusema atafanya Mungu, heey, atafanya endapo na wewe utafanya. Mungu amekupa kila kitu anachohitaji ni wewe kuvitumia vile alivyokupa, yeye ni kama Mwongozo kwako na kukulinda lakini tegemeo lake ni kwamba  katika kukulinda kwake anategemea wewe kutumia vile alivyokujalia. Mungu ametuweka katika ulimwengu wenye maarifa, hekima, mafanikio makubwa n.k hajaweka kulipishwa kodi kuvichukua hivi vitu wala hajaweza risiti za kupewa baada ya kulipiwa ni wewe mwenyewe tuuu. Kumbuka hata unavyolalamika kwamba mbona maisha yako hayabadiliki sio kwamba hakuoni anaona na anakuangalia zaidi atashangaa wewe kutokuvitumia vile alivyokujalia kuwa navyo licha ya kwamba kutakuwa na changamoto lakini hivyo sio vipaombele katika maisha yako. 

"Mungu atatengeneza njia pale pasipokuwa na njia" lakini kumbuka hawezi kutengeneza njia na kukupatia kama wewe mwenyewe hujajiandaa kutembea katika hiyo njia, hawezi kukutengenezea hiyo njia kama hujajiandaa kihekima na kuwa na maarifa pamoja na kuwa kiongozi wa wewe mwenyewe. Utashangaa kila siku unajitahidi sana kusali na kuzungukwa na watu ambao wamefanikiwa lakini bado njia yako haionekani, sababu inaweza kuwa kwamba kimwili uko na hao watu lakini ndani yako bado maandalizi ya kukabidhiwa hiyo njia na Mungu bado na Mungu anakuangalia na kujiuliza lini huyu ataanza kuwa tayari? 

Nikirudi mwanzo katika usemi wa Iman Hasan Ali Shah changamoto ni lazima katika kila jambo ambalo unalifanya haswa jambo jema, ukiweka katika akili yako na kutambua hili katika kila jambo ambalo unalifanya  Amini hauko mbali katika mafanikio yako.Cha msingi ni kwamba tusiombee changamoto ila mwombe Mungu wako kuweza kukupa nguvu za kupambana nazo mana changamoto hata siku moja hauwezi kukwepa hata Mungu anajua hilo angalia wana wa Israel ambao ni Taifa teule kwa Mungu walipata changamoto kutoka kwa Wafilistini haijatosha, haijatosha bado walikuwa watumwa kule Misri kwa miaka zaidi ya 100 walikaa jangwani kwa miaka 40 hizi zote ni changamoto lakini mwisho wa siku nchi ya AHADI waliweza kuiona. Unadhani waisrael waliomba kuondokana na changamoto kupitia viongozi wao? hapana, ila waliomba nguvu ya kuweza kuzishinda. 

Muhimu.

Kubali Mungu wako Akuhamasishe kwanza kabla ya binadamu Kukuhamasisha. Hapo utapata hamasa ya kwelii ila ukianza na binadamu alafu ikafuata Mungu utakuwa unajidanganya sana. Na kumbuka Mungu anatengeneza njia pale ambao panaonesha kwamba kunauhitaji wa kwelii wa hiyo njia, inaweza kuwa njia ya kuwa pastor, mkulima, mfanyabiashara, mhamasishaji, mwandishi, mfanyabiashara au mjasiriamali,hivi vyote itategemeana na maandalizi ya tabia zako mana hakuna mabadiliko yoyote ambayo unaweza kuyapata katika maisha yako bila kubadili tabia kwanza na hakuna mazingira yoyote mazuri duniani unaweza kuyapata bila kutemgeneza tabia ambayo itavuta yale mazingira ambayo unayahitaji katika maisha yako.

By LAZARO SAMWEL
CONTACTS : 0753616584 / 0653386586 
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com

FACEBOOK PAGE ; Lazaro Samwel 
INSTAGRAM          ; Lazaro_samwel3


0 comments:

Post a Comment